preloader
Edit Content

Our Location

We are a Specialised Polyclnic located at Karatu area in Arusha Region. 

Contact Info

Kliniki Ya Daktari Bingwa – Magonjwa ya Ndani

  • Home
  • -
  • Ijue Afya Yako
  • -
  • Kliniki Ya Daktari Bingwa – Magonjwa ya Ndani
Kliniki Ya Daktari Bingwa – Magonjwa ya Ndani

Daktari Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani ni daktari ambaye anajishughulisha na matibabu hasa ya magonjwa ya ndani ya mwili kama vile moyo, figo, mapafu, na ini. Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani pia ana ujuzi wa kushughulikia magonjwa kama kisukari, shinikizo la damu, na kansa.

Ni muhimu kwa watu kutembelea hospitali na kuonana na Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani ndani wanapojisikia wagonjwa au hatakama siyo wagonjwa kwa ajili ya kukagua afya na kuepuka athari za maradhi ya baadae ambazo zingeweza kugundulika mapema na kutibiwa kwa wakati. Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani anaweza kusaidia kugundua mapema magonjwa na kutoa matibabu sahihi. Pia, anaweza kusaidia kuzuia magonjwa kwa kutoa ushauri wa lishe bora, mazoezi, na uchunguzi wa mara kwa mara.

Ni muhimu kuona na Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani mara kwa mara ili kudumisha afya yako na kugundua mapema magonjwa yoyote. Usisubiri hadi uwe mgonjwa sana ndipo uende kwa daktari. Inashauriwa kuwaona Madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani angalau mara moja au zaidi kwa mwaka ili kudumisha afya yako na kuepuka matatizo makubwa ya kiafya.

JJ Polyclinic Karatu, tumekuwa pia tukitoa huduma ya kuonana na madaktari bingwa ikiwemo Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani, akina mama na uzazi, mifupa n.k. Kwa mawasiliano unaweza kutupigia kwa namba 0762 858 888, au kufika kituoni kwetu. Karatu mjini, Mkabala na benki za CRDB na NBC, pembeni ya mgahawa wa mushroom.

Unaweza pia kupiga simu au bonyeza HAPA kuangalia ratiba za clinic za madaktari bingwa kwa wiki au mwezi husika.

Kutakuwa na Kliniki ya DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA NDANI: MOYO,FIGO,PRESSURE,KISUKARI NA MENGINEYO. 27/04/2024 Siku ya JUMAMOSI. Wote mnakaribishwa.
AFYA NI MTAJI, AFYA NI MAISHA, AFYA NI UHAI. NJOO UPIME AFYA YAKO

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *